0

Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka.

Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac).

Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo.

“Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,”alisema.

Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi.

Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu ugonjwa huo kuliko wanawake.Hata hivyo, alisema kwa sasa ipo kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kuwataka wabunge na viongozi mbalimbali kutoa elimu juu ya kujikinga na gonjwa hatari la ukimwi.

Aidha Mrisho alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa asilimia 14.8 ambapo Unguja Kaskazini inamaambukizi madogo kwa asilimia 0.1.

Hata hivyo alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na rasilimali za ukimwi kwa serikali, mashirika ya Dini na sekta binafsi kuwa pungufu kuliko mahitaji.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto lakini nia ni kufikia sifuri tatu ifikapo mwaka 2015 na hiyo hipo katika ulimwenguni, Afrika hapa hapa Tanzania.

NIPASHE

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X