Pamoja na kuwa na RASIRIMALI nyingi ikiwemo Madini
aina mbalimbali, Misitu ya kila aina, Barabara iunganishayo Nchi jirani
kama Uganda, Rwanda na Burundi, Hifadhi ya ushirombo, Vyanzo vya maji
kila kona ya Runzewe, tuko na kila aina ya Rasirimali. Maajabu ya dunia,
mpaka leo bado tunamatatizo lukuki kama:-
a. Uhaba wa maji ktk
mji wetu hasa kuanzia miezi y jully mpaka November, mf mwaka jana dumu 1
la lita 20 liliuzwa mpaka Tsh 500...!
b. Uhaba wa NISHATI muhimu
kama umeme wakati mji unastahili kuwa na Umeme, ingawa kuna tetesi kuwa
eti kuna mashimo ya nguzo yanachimbwa.
c. Pamoja na kuwa na bw
Afya lakini mazingira bado ni machafu, zunguka maeneo ya MASANKURONI,
MACHINJIONI, hapo LAMI karibu na wauza mahindi, hata kwenye hii mitaa
SOKOMJINGA kuel...ekea kwa baraka.
c. Miundombinu mibovu,
mf, hayo masoko yetu yaliyojengwa kwa nguzo za Mbao na mabati yake
kuegeshwa tu, uchakavu wa mabomba ya maji na matanki kitu ambacho ni
hatari kwa maisha na afya za wakazi.
e. Ukosefu wa ajira kwa
vijana tuliowengi hasa hawa wanaohitimu kwny shule na vyuo badala yake
wengi kukimbilia UNGONI(wachimbaji wadogo) kazi ambayo haina masirahi zaidi ya kuteketeza
vijana wengi kwa wimbila UMALAYA.
f. Ufisadi na dhuluma, ninayo
mifano, kwa huyu bwana afya alikuwa akitoa ZABUNI kwa wenye MATELA na
kujili BIBI zetu na hatima yake ni kuwadhulumu tu( sina hakika kama bado
yupo), Ufisadi mwingne ni pindi ya kuuza VIWANJA hasa kwny Masoko yetu,
eti mpaka mtendaji apate kidogo ndiyo upate kiwanja.
g. Huduma
za Afya bado ni mbovu hasa kwny hii hosipitali ya serikali, eti vipimon
then dawa hamna, Pongezi kwa Dr BARAKA na hosipitali yake.
TATIZO
NINI Ndg zanguuuuuu....? Ninayo mengi saana ila naomba kwanza TUCHANGIE
KWA HAYA MACHACHE ikiwezekana NJOO na SULUHISHO la MATATIZO YA
RUNZEWE........
Ujumbe huu umeandikwa na Mr Peter Mayala kupitia group lao liitwalo Runzewe Development Group (RDG)
umepatia sana Shebby blog kweli tuna majanga sana Runzewe
ReplyDeletenimeipenda sana hii wana Shebby D blog endeleeni kuitangaza Runzewe popote ijulikane pote
ReplyDelete