Home
»
KIMATAIFA
» MTOTO WA KIKE WA MANDELA AWAJIA JUU WAANDISHI WA HABARI WALIOPIGA KAMBI NJE YA HOSPITAL ALIYOLAZWA MANDELA
 |
Mtoto wa kike wa Mpiganiaji Uhuru wa South
Africa Nelson Mandela anaeenda kwa Jina la Makanziwe Mandela,Juzi
aliongea kwa ukali na kutoa tamko juu ya waandishi wa habari
waliopiga kambi nje ya hospital ambayo Baba yake kwa sasa amelazwa akipigania
maisha yake kutokana na matatizo ya mapafu.....
Hali hiyo imekuja baada ya vituo vya
habari kuweka kambi nje kwenye hospital hiyo iliyopo Pretoria.... Makanziwe
akiongea kwenye simu kumjuza mwandishi wa habari wa Ikulu kuhusu
Hali ya mzee mandela aliongea hivi ''Tunashukuru Mungu baba kwa sasa
hali inaridhisha, ni mtu mzima sana lakini Mungu anazidi kutupigania
na familia tunaamini atarudia hali yake kama zamani na kujongea na
sisi nyumbani....
Akizidi kuongea,ndipo alipofunguka juu ya
waandishi wa habari ''Nachukizwa na kitendo hiki cha hawa waandishi
wa habari kabisa wanadiliki kuweka kambi nje ya hospital kuripoti
hali ya baba yangu,kusema kweli sijapendezwa au kwa kuwa sisi ni
waafrika ndio atupaswi kueshimiwa tunapoitaji undani
wetu,nimechukizwa sana yani wapo nje kana kwamba wanasubiri kitoke
kitu wawe wa kwanza kuripoti...... Alizidi kusema ''Tunahitaji
undani wetu kukiwa na jambo lolote familia itawajuza naomba heshima
itumike na busara kwajili ya mzee wetu,sidhani kama angekuwa yupo
katika hali nzuri angefurahia kuona kitu kama hiki''
Hayo
ndiyo yaliyosemwa na Mtoto wa kike mkubwa wa Nelson Mandela..... |
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment