MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi
(SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa
dhamana.
Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma
anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika
vikao vya Bunge.
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika
Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na
baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni
hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.
Hata hivyo taarifa za awali za tukio la
kukamatwa kwa Mbunge huyo wa
Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na
kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
Habarim
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment