“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya kupata habari hizo mwandishi wetu alimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
mwadishi- Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment