0

NCHIMBI
 78275
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa siku mbili wa viongozi wa dini na wajumbe  wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, juzi usiku.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi  amepiga marufuku mikutano ya hadhara isiyokuwa na vibali maalumu vya vyombo vya dola.
Kauli hiyo  imekuja siku moja baada ya viongozi wa dini, kutaka mikutano ya hadhara isifanyike bila kufuata taratibu za kisheria.

Waziri Nchimbi pia amewaagiza makamanda wa polisi kote nchini, kuwafuatilia kwa karibu watu watakaokiuka agizo hilo na kuwachukulia hatua za kisheria.
Dkt. Nchimbi alitoa agizo hilo juzi usiku jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza  katika mkutano wa viongozi wa dini.
Alisema kamanda yeyote wa polisi atakayeshindwa kudhibiti tatizo hilo, atakuwa wa kwanza kuwajibika katika eneo lake la kazi.
Akizungumzia kusambaa kwa maneno ya uchochezi  kupitia mitandao ya kijamii alisema: “Ninaomba wazazi tuwaonye watoto wetu na vijana wetu wanaotumia mitandao hiyo vibaya kwani kama itaendelea kuachwa itumike ovyo, itaharibu amani tuliyokuwa nayo kwa zaidi ya miaka 50,” alionya Nchimbi
Katika hatua nyingine, alibainisha kwamba kwa sasa Serikali na vyombo vya usalama vinafuatilia mawasiliano ya simu yanayofanyika hasa yanayolenga kueneza  masuala ya udini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema wamefikia maazimio 16 yaliyotokana na kikao cha majadiliano ya viongozi wa dini huku kubwa likiwa kudumiasha amani ya mkoa huo na taifa kwa jumla.
Maazimio hayo ni kutokuruhusu amani kuchezewa, viongozi wa dini wajihadhari na matamko yanayoweza kuleta mfarakano miongoni mwa jamii na waheshimu imani za wengine. Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X