Bomu
lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa
lilitengenezwa kienyeji.
Wakati
kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina Kurusei, (45),
James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika leo
Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.
Ofisa
mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye hakutaka jina
lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi
na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi
wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya
20.
Watu saba
wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.
Mstaafu
huyo alieleza kuwa mabomu mengi zaidi ya kienyeji hutengenezwa kwa
kutumia bakuli za chuma, zikiwekewa baruti ndani na kufungwa kwa waya.
"Hawa
jamaa huweka vipande kama 36 vya baruti na hufungiwa ndani ya bakuli kwa
kubanwa sana ili kuvipa joto na bomu likitua, husababisha madhara
makubwa," alisema ofisa huyo ambaye alishiriki Vita ya Uganda mwaka 1978
hadi 1979.
Mstaafu
huyo alisema mabomu ya aina hiyo yametumika kwenye mashambulizi ya
kigaidi katika nchi mbalimbali duniani kama Lebanon, Vietnam, Libya,
Ireland Kaskazini, Syria, Afghanistan, Iraq, Chechnya na India.
Mmoja wa
majeruhi, Mwalimu Fatuma Tarimo amesimulia alivyoshuhudia bomu likitua
mbele yake na kulipuka.
Tarimo,
ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alisema jana
kuwa aliliona bomu hilo likiwa na rangi ya shaba. Pia alisema lilikuwa
na waya kwa juu.
"Baada ya
kutua, nilisikia kishindo kikubwa nikashtuka ikabidi niangalie. Baada
ya kuona ni kitu kama chuma nilipata hofu nikafikiria kuondoka," alisema
mwalimu huyo wa Shule ya Msingi ya Burka Estate, nje kidogo ya Jiji la
Arusha. Hata hivyo, alisema kabla ya kuondoka, alishtukia amenyanyuliwa
juu na hakujua kilichoendelea kwani aliposhtuka alijikuta akiwa katika
Hospitali ya Mount Meru.
Tarimo
ametolewa kipande cha chuma katika mguu wake wa kulia.
"Nina maumivu bado lakini nina matumaini nimechukuliwa kipimo cha 'T-Scan' kwa matibabu zaidi," alisema Mwalimu Tarimo ambaye anaaminika kuwa na kipande kingine kwenye mapafu.
"Nina maumivu bado lakini nina matumaini nimechukuliwa kipimo cha 'T-Scan' kwa matibabu zaidi," alisema Mwalimu Tarimo ambaye anaaminika kuwa na kipande kingine kwenye mapafu.
Majeruhi
mwingine, Jenipher Joackim ambaye amefiwa na mwanaye Patricia Joackim
(9) hana taarifa za kifo hicho kilichotokea katika Hospitali ya KCMC.
"Nimeambiwa kwamba yupo ICU sijui anaendeleaje," alisema.
"Nimeambiwa kwamba yupo ICU sijui anaendeleaje," alisema.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment