Kocha wa Everton anayemaliza muda
wake, David Moyes akienda kuaga kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bill
Kenwright leo alasiri.
Hapa Moyes akiingia ofisini kwa
Kenwright kwa ajili ya mazungumzo ya kumuaga ili akasaini mkataba wa
kuinoa Manchester United.
Moyes akitoka nje ya uzio wa ofisi ya
Kenwright, baada ya kukamilisha mazungumzo ya kumuaga.
Huyoooooo akichanja mbuga kwa furaha
baada ya kukubaliwa kuihama klabu hiyo akiwa amebakiza mktaba wa wiki
sita .
Hapa kocha huyo 'anatroti' huku
akionekana kama anayesema: Ngoja niwahi, wasije Man United wakachomoa
kunipa ulaji bure!
Ni kama anasema: Siamini kama issue
itakwenda kama navyotarajia.
MANCHESTER, England
Moyes, 50, ameingia mkataba wa miaka
sita kuifundisha Manchester United, kujaza nafasi inayoachwa na Sir Alex
Ferguson, aliyetwaa zaidi ya mataji 30 akiwa na Mashetani Wekundu hao,
yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya hapa
KLABU ya Manchester United, imeingia
mkataba wa miaka sita na kocha wa Everton anayemaliza muda wake David
Moyes, ili kujaza pengo linaloachwa na Sir Alex Ferguson.
Ferguson, 71, juzi alitangaza
kustaafu kuinoa Man United mwishoni mwa amsimu akihitimisha miaka 26 ya
kufanya kazi na klabu hiyo Old Trafford.
Kutokana na uthibitisho wa Man United
kumpa mkataba Moyes, aliyebakiza wiki sita kwenye mkataba wake na
Everton, kocha huyo anahitimisha miaka 11 ya kuinoa klabu hiyo yenye
makazi yake Goodison Park.
Moyes, 50, ameingia mkataba wa miaka
sita kuifundisha Manchester United, kujaza nafasi inayoachwa na
Ferguson, aliyetwaa zaidi ya mataji 30 akiwa na Mashetani Wekundu hao,
yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya hapa.
"Sisi kwa kauli moja tumekubaliana na
David Moyes," alisema Ferguson.
"Moyes ni mtu mwadilifu, mwenye
maadili imara ya kazi. Nimekuwa mfuasi wa kazi zake kwa muda mrefu na
nilimtaka aje hapa waka 1998 kujadili naye juu ya nafasi ya kocha
msaidizi.
"Hakuan maswali juu ya hili, ana sifa
na viwango vyote tunavyotarajia kutoka kwake kama kocha wa klabu hii,"
Fergie alimuelezea Moyes.
Alasiri jana, Everton ilithibitisha
katika taarifa yake kuwa: "Everton inathibitisha kuwa Moyes ataondoka
klabuni Goodison Park mwisho wa msimu.
"Alikutana na Mwenyekiti Bill
Kenwright mapema alaasiri ya leo na kuthibitisha kuwa anataka kujiunga
Manchester United.
"Mwenyekiti kwa niaba ya klabu,
anapenda kutoa shukrani za dhati kwa Moyes kwa rekodi mbalimbali
alizoweka tangu kutua kwake hapa Machi 2002," ilisomeka taarifa ya
Everton.
Ferguson, ambaye atabaki klabuni Old
Trafford kama Mkurugenzi na Balozi, amekuwa na uhusiano wa karibu mno na
Moyes ambaye aliwahi kupendekeza awe msaidizi wake wakati huo Moyes
akiwa anainoa klabu ya Preston North End.






Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment