Nasibu
Abdul “Diamond Platnumz” akiwa katika pozi mjini Reading anapoendelea
na ziara yake.
TAFSIRI ya neno Diamond kwa kiswahili ni Almasi ambayo ni moja ya
madini yenye thamani kubwa. Bila shaka mwanamuziki Nasibu Abdul
“Diamond Platnumz” analitendea haki jina hilo, nalo pia linamtendea
haki. Msanii huyo wa Bongo Flava mwenye uwezo mkubwa jukwaani ni
miongoni mwa wanamuziki wenye mashabiki wengi Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla. Mbali na jina hilo, pia anafahamika kama rais wa
Wasafi na sukari ya warembo.
Katika pitapita za mitaani, imegundulika kwamba jina lake pia
limezaa majina mengine mawili ambayo ni Dai-mond na Dia-mond. Ni majina
ambayo yanasikika kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake wanaoshindwa
kulitamka jina lake vile inavyotakiwa.
Diamond ambaye kwa sasa yuko nchini Uingereza, mwaka huu yuko
kwenye tuzo za muziki wa Tanzania “Kilimanjaro Tanzania Music Awards”
kwenye vipengere vya msanii bora wa kiume kwa ujumla na msanii bora wa
kiume Bongo Flava.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment