jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa
Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya
ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.
Akihojiwa
katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa
bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na
fans wa Tanzania, na pili
ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa
sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia
jana
(April 30) pale Elements club.
Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa
yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina
yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya
Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa
marafiki
wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote
kati yangu na diamond na sijaja Tanzania kufuata penzi lake...
we
are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship
katika muziki", alisema Avril.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment