Baadhi ya wananchi wanaohudhuria vikao vya bunge mjini hapa wanasema wabunge hao, hasa wa Chadema na CCM wanapokuwa ndani ya mjengo ni maadui wakubwa, wakahoji:
Lakini mbona wakitoka nje wanachekeana sana, tena marafiki au wanatuzuga wapiga kura wao tuwaone wako siriasi?”
Mmoja akaendelea: ”Mimi naamini kwamba wanapokuwa nje ya bunge ni marafiki na wanapokuwa mjengoni wanachofanya ni kulinda itikadi zao za kisiasa tu, hakuna lingine.”
Akaendelea kuwa, wananchi wengi huamini kwamba waheshimiwa ni maadui wa moja kwa moja, hasa wanapowaangalia kwenye tivii wakibishana mbele ya spika wao, Anne Makinda lakini ukweli si maadui.
Uwazi lilinasa baadhi ya picha zinazowaonesha waheshimiwa ‘maadui’ ndani ya bunge wakichekeana kwa ‘meno 32’ nje.
Picha hizo ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Lukuvi
akiwa na Mnyika.
Hata hivyo, Lukuvi amewahi kusema: “Ndani ya bunge wabunge wote
wanafanya kazi kwa masilahi ya wananchi na taifa kwa ujumla, hakuna
uadui.”Aidha, kuna picha ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Tundu Lissu na Spika Makinda wakicheza muziki, Lukuvi na Lissu wakibadilishana mawazo, Mnyika, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe pia wakibadilishana mawazo.
Picha yenye kutia fora ni Mbunge wa Bunda ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), Steven Wassira ‘Tyson’ na Mbunge wa Arusha Mjini kwa ‘leseni’ ya Chadema, Godbless Lema.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment