Good news ninayotaka kukusogezea ni hii
kutoka kwa Joh Makini na G Nako ambao wapo Afrika Kusini Johannesburg
kwenye maandalizi ya video zao.
Joh Makini akiamplify kwenye AMPLIFAYA
ya Clouds FM Agosti 25 alithibitisha kufanyika kwa video 3 ikiwemo yake
na rapper A.K.A wa South Africa.
‘Kila kitu
kimeenda sawa, kila kitu kimeenda jinsi tulivyopanga namshukuru Mungu
kwa maana yeye ndio amefanikisha sisi tuweze kufanikiwa ku shoot video
za single zenu kwa takribani siku tatu ukichukulia kama wiki tuko huku
Johannesburg na tayari tumeshafanya video tatu kwa hiyo watu wakae
tayari kwa ujio wa G Nako na Joh Makini’ – Joh Makini
‘Kuna
video ambayo mimi na rapper AKA wa South Africa halafu kuna video ya G
Nako pekee yake ambayo inaitwa Original na kuna video nyingine ambayo
mimi nimeshirikishwa na binti mmoja mwimbaji kutokea Tanzania ambaye
naye anakuja kwa hiyo vitu vingi vikubwa vinakuja kama nilivyokuambia
tupo katika vibe ya kimataifa zaidi na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kila
kitu kinaenda sawa dua zetu muhimu katika kuipeperusha Bendera ya
Tanzania’ – Joh Makini.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment