Ni mwaka wa Uchaguzi Tanzania ambapo
upinzani mkubwa unaonekana kwenye Wagombea wawili ambao ni John Pombe
Magufuli atakaegombea kupitia CCM na Edward Lowassa aliyechukua fomu ya
CHADEMA kwenye headlines za muungano wa vyama vya upinzani (UKAWA)
Tayari mpaka sasa tumeona baadhi ya
mastaa wa Tanzania wakiweka wazi watu wanaowakubali kati ya hawa wawili,
miongoni mwao ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli,
mwigizaji Jackline Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa
na sasa ni Diamond kaweka wazi.
Diamond anamsupport John Pombe Magufuli na kayaandika haya >>> Iwe
Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya
Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo
ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya
tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio
Jembe’
Kwenye sentensi ya pili Diamond akaandika >>> ‘Nitakuandikia
na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli
Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye
karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue
Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa
sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako
nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment