Kufuatia tukio la vurugu kubwa zilizotokea wakati wa show ya Diamond Platinum huko Stuttgart, Ujerumani, promota wa kampuni ya Britts event ameutumia ujumbe uongozi wa Diamond.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Babu Tale ameeleza kuwa
promota huyo amewatumia barua pepe kuwaomba radhi na wao wamemuelewa na
kumsamehe.
“Promota ametupigia simu kuapologize ametuma na email, sisi kama binadamu tumemuelewa na tumemsamehe.” Amesema Babu Tale.
Akieleza jinsi alivyolichukulia tatizo hilo, amesema kuwa yeye anaona kama sio hasara na analichukulia kama sehemu ya exposure.
“Matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ukichukulia
matatizo kama hasara utakuja kujuta bure. Unachukua kama xposure,
unajifunza. Mwisho wa siku sisi tulikuwa tumelipwa hela yetu yote ya
kazi na kila kitu. Athari kubwa aliipata yeye kwa sababu watu walikuja,
ukumbi unamdai na nini. Na sisi kama binadamu tumeishia tu kumuonea
huruma na kusema aaah ngoja turudi kwetu.” Babu Tale ameiambia The Jump
Off.
Akizungumzia ahadi ya kampuni ya Britts kumrudisha tena Diamond
Ujerumani na kufanya show itayoshuhudiwa na mashabiki bure, Babu Tale
wanasubiri kutoka kwa promota huyo na kwamba watakapopata uhakika
wataeleza.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment