kiongozi wa kundi la kigaidi la Al- Qaeda, Ayman Al-Zawahiri ametoa tangazo kuwa kundi hilo limefungua tawi jipya nchini India.
Kwa kujibu wa BBC, katika tangazo hilo lilitolewa kupitia kipande cha
video linaeleza kuwa nia ya kuanzisha tawi hilo ni kutaka kuhakikisha
wanapandisha bendera za Jihad kusini mwa bara la Asia kama walivyoweza
katika maeneo kadhaa nchini Iraq na Syria kupitia kundi la ISIS.
Tangazo hilo linakuja ikiwa siku mbili baada ya majeshi ya Marekani
kueleza kuwa yamefanya mashambulizi ya kushitukiza dhidi ya kundi la
Al-Shabaab ambalo ni washirika wa Al-Qaeda na inawezekana lilisababisha
kifo cha kiongozi mkuu wa kundi hilo ambaye yuko katika orodha ya watu 8
wanaotafutwa zaidi duniani na Marekani.
Hata hivyo, Marekani ilisema inafanya uchunguzi kufahamu kama walimuua kiongozi huyo ambaye hata picha yake haijawahi kuonekana.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment