JE, unamfahamu mtu aliyetunga sauti (melody) ya wimbo ambao
leo Watanzania wanauita Wimbo wa Taifa?Huyu ni Enock Sontonga, raia wa
Afrika Kusini, aliyetunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’
ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’
iAfrika’.
Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905.Sauti ya
wimbo huo imetumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za Afrika
Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania – ambapo Tanzania na
Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii.Nchi zingine tatu
za Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini zimetunga nyimbo nyingine.
Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897 na kurekebishwa na wahariri
mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa. Kwa
habari zaidi fungua mtandao sehemu ya (Wikipedia) kupitia:
http://en.wikipedia.org/wiki/Enoch_Sontonga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment