Msanii
wa Hip Hop kutokea Mwanza, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amesema kuwa
majanga anayopata kwenye mahusiano yake yanatokana na kutompata mwanamke
anayemhitaji.
Akizungumza na Mkasi TV hivi karibuni, Dudu Baya amesema wanawake wengi anaokutana nao wanakuwa ni machizi.
“Kwanza
sijabahatika kukutana na mwanake ambae mimi namtaka, nafikiri Mungu
bado hajanipa huwaga nakutana na machizi, kwa sababu mimi sipendi,
mwanamke aliyelelewa na kufundwa vizuri vitu vya ndani huwezi ukavitoa
nje.
Kwa
mimi binafsi siongeagi kwa wanaume wengine, napenda sana siri za
familia zibaki kuwa siri za familia. Kwa mfano huyu jinsi alivyoenda
kwenye media asitarajie nimtamrudia kabisa, ile tabia ya kwenda kwa
jirani na kanga moja ikianguka? Kweli kabisa kicheni party zinaendelea
lakini hazisaidii kitu chochote,” alisema.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment