Wanakijiji hao walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji
kugongwa na uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa
kengele hiyo kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na
watu wasiojulikana.
Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya
wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele
kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.
Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta
mganga kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja
aliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Hata hivyo, walitahadharishwa kwam
ba kama aliyeshiriki hatakunywa dawa hiyo, itamuumbua maana aliyeibiwa atakuwa amekunywa.
ba kama aliyeshiriki hatakunywa dawa hiyo, itamuumbua maana aliyeibiwa atakuwa amekunywa.
Kabla ya kuanza kunyweshwa, mganga huyo aliomba wanakijiji iwapo kuna
mhusika, ni vyema ajitokeze kabla ya kuingia gharama za kuwarejesha
hali yao ya kawaida hazijaongezeka watakaponaswa.
Hata hivyo, wanakijiji walidharau wakidai ni mbabaishaji huyu hawezi lolote kwani hivyo ni vitisho.
Ilipotimu saa 5:00 asubuhi, mganga aliwaeleza ndani ya saa mbili
tangu mtu anywe dawa yake atakuwa ameanza kuonyesha vitendo alivyokuwa
akifanya wakati anaiba dukani.
Saa 6:00 mchana tayari dalili zilikuwa zimenza kuonekana kwa watu
saba wakiwamo wafanyabiashara wenzake, pia yumo mwanamke wakiwa wamelewa
wanafanya vioja, huku wengine wakila nyasi na kutafuna midomo.
Wambura alisema anachotaka ni kurejeshewa Sh12 milioni, zikiwamo
gharama za mganga huyo, huku walionaswa na dawa hiyo wakitakiwa kulipa
Sh3 milioni na kupewa siku tatu vinginevyo watageuzwa vichaa.
“Nimeibiwa sana ila ninavumilia, hii ni mara ya tano sasa, nimechoka
na ninachotaka wanirudishie Sh12.5 milioni gharama niliyotumia ikiwamo
mali zangu walizochukua, waliwahi kunivamia na mke wangu tunatoka dukani
wakatukata mapanga hadi mke wangu akafa,” alisema Wambura.
Pia, tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Mji wa Tarime, Vanance Mwamengo, madaktari wa Hospitali ya Mji wa
Tarime, madiwani na polisi na kwamba kutokana na wananchi kutokuchukua
sheria mkononi, masuala hayo yatamalizwa kimila.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment