Kijana
mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kwa kupigwa
mawe kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya
kukamatwa na pikipiki ya wizi Katika kijiji cha kagongwa Wilayani
Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo
limetokea jana majira ya saa nane Mchana mara baada ya marehemu kuiba
Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba
mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana Asubuhi Maeneo ya
shule ya Kahama Musilim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija
Zacharia.
Kwa mujibu
wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm Kuwa
alipewa taarifa na dereva wake ambpo aliamua kutoa tarifa ya upoteza
pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na Kagongwa.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment