Na mwandishi wetu.
Conrad
Kwa miongo kadhaa sasa mji wetu ume kuwa ukitegemea kipato kutokana na shughuli za uchuuzi wa madini ya dhahabu kutoka kwa vijana almaarufu kama NGONI japo hamna alitokea RUVUMA-Songea. wanako ishi watu kabila la Wangoni.
Kiuhalisia kwa sasa hali ya utendaji na uingizaji wa Shilingi hapa mtaani kwetu ime kuwa ngumi tena Ngumu sana baada ya NGONI hao kupigwa marufuku na kuwekewa ulinzi mkali huko POLI. Yaani kiufupi mzunguko wa hela umepwaya sana. Hela ilizunguka kwa Mfumo kama huu
Bodaboda
Ngoni
Wenye baa na wauzaji wa mvinyoo wengine
Wenye Nyumba za Wageni.
Mama Ntilie
Wauzaji wa maji.
kwa utaratibu huu RUNZEWE yetu ilikuwa na hekaheka za kila mtu
kutafuta fedha ambayo ilikuwa inapatikana hapa kwetu.
baada ya kuwazuia Ngoni runzewe ime poa hadi kufukia watu na wakaazi wengine kuamua kuhama. Yaani wamefunga bidhaaa na shughuli zao walizo kuwa wakifanya awali.
Jamani wanaRunzewe tufanye nini kurudia hali yetu ya awali kukidhi kuyamudu maisha yetu ya kila siku?
je, tuwavamie walinzi wa mgodi? jibu ni hapana kwani italeta maafa
je, tuandamane hadi wizara ya KAZI na AJIRA? itachukua muda kupata sitahiki zetu.
basi ni muda sasa wa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato hapa mtaani kwetu.
vyanzo hivyo ni kama....
Uchuuzi wa mazao
Uoteshaji wa miche ya miti na maua.
na nyingine nyingi kama zilivyo aniinishwa na wizara ya Kazi na Ajira.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment