Info kamili kuhusu bondia Evander Holyfield kuletwa Tanzania
PromotaMtanzania Jay Msangi kutoka Hall of Fame Boxing and Promotions Company ameongea na kusema hilo game limepangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa April 27 2014 Uwanja wa Taifa ambapo Evander atapiga na na Francois Botha wa South Africa aliewahi kuwa bingwa mara mbili.
Jay amesema haijawa ngumu kumpata Evander kwa ajili ya pambano kwa sababu kampuni yake ina uzoefu wa miaka mingi na imeshaandaa mapambano zaidi 30 kwenye jimbo la Ohio Marekani, ni kampuni ambayo iko Marekani na hapa Tanzania.
Hata hivyo kwa mara ya kwanza hii kampuni August 30 2013 itamkutanisha bondia Francis Cheka na Mmarekani Derrick atakaekua bondia wa kwanza Mmarekani kuja kupigana Tanzania.
Siku hiyohiyo ya August 30 pia mabondia Mada Maugo na Thomas Mashari watashuhudiwa wakizichapa live.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.