Baada
Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo
pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo
yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua,
hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya
wale walioonekana kukaidi agizo hilo.
Katika kutekeleza agizo hilo zoezi
hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo
eneo la Victoria .
Msongamano pande hizo.....
Tayari
ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani huku baadhi ya
watu wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha
baadhi ya vifaa.
Wakati likianza zoezi hilo ndani walikuwapo watu wanaoendesha shughuli
zao katika jengo hilo.
Baadhi ya wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakiduaa wasijue la
kufanya.......
Umeshashushwa upande mmoja.
Huu ni upande wapili wa jengo hilo.
Ni upande wa mbele wa jengo hilo zima unavyoonekana....
Jamaa
wakisimamia usalama pande hizo wakiwafukuza raia waliokuwa
wamekusanyika eneo hilo na kuongoza magari kuondoa foleni eneo hilo.....
Katapila
likiendelea na kazi ya kubomoa hapa ni jengo la pili lililokaribu na
Green Acres nalo likiliwa hapa tayari ukuta ukiwa unashushwa.....
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment