Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene zimesema kuwa uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Bw.Makene
 ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  
vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao 
wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na 
watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama
 tawala.
Viongozi
 hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya 
kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia 
rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani 
inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment