MREMBO
asiye na majivuno kunako anga la filamu Bongo, Esha Buheti amenawa
mikono kwenye ulingo wa filamu kutokana na kuchoshwa na malipo kiduchu
anayoyapata kwenye tasnia hiyo na kugeukia kwenye mambo ya ujasiriamali.Akipiga stori na Amani, Esha alisema kuwa kuna mambo mengi yamekuwa yakimkwaza kwenye tasnia hiyo likiwemo suala la malipo, isitoshe tasnia ya filamu imeshuka kwa kuwa kazi nyingi sokoni zinagongana zikiwa na ladha moja ya mfumo wa maigizo.
“Nimeamua nijikite kwenye biashara, naanza kwa kufungua mgahawa na tayari nimeshapata wadhamini. Kwenye sanaa kuna vitu vingi nimevivumilia lakini nilichoambulia labda ni kushushwa thamani tu kwa kile kinacho
onekana wasanii hatujatulia,” alisema Esha.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment