
Hadi
sasa kuna baadhi ya mastaa wa Tanzania, wameweka wazi watu
wanaowakubali kati ya wagombea wawili, miongoni mwao ni Wema Sepetu
aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, muigizaji Jacqueline Wolper na Aunty
Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond ameweka wazi
kuwa yupo team Magufuli.
Kupitia
mtandao wa kijamii Diamond ameandika “Iwe Msanii, Mtangazaji, ama
Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini
ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi
yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni
zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio Jembe,”.
Akamalizia
“Nitakuandikia na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona
John Magufuli Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea
umtakaye karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila
usijisumbue Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha
akili yangu kwa sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea,
nipe fact zako nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu
#Ccm,”.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment