MAMLAKA ya hali ya hewa nchini (TMA), imewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo ya Ukanda wa Pwani.
Taarifa
iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mamlaka hiyo, ilisema mvua hiyo
itanyesha kwa zaidi ya milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Januari 18
hadi 20 mwaka huu.
Maeneo
ambayo yataathirika na mvua hizo ni Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi,
Morogoro, Pwani, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja, Zanzibar.
"Hali
hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa eneo la Bahari
ya Hindi Mashariki mwa Kisiwa cha Madagasca hivyo kusababisha ongezeko
la unyevunyevu kutoka misitu ya Congo," ilifafanua taarifa hiyo.
Kutokana
na hali hiyo, wakazi waishio katika maeneo hatarishi kama mabondeni ni
vyema wakachukua hatua zinazostahili ili kuepuka madhara.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment