Kulala na
wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani
ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.Katika utafiti uliochapishwa
katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal
wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika
maisha yao yote, kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa
kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume
3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590
walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka
2009.
Kwa jumla
watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha
mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao
wenye saratani.Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume
anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata
ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina
yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment