0


Soko  la  vinyago  lililoko  karibu na  ofisi ya   CCM   wilaya   ya   Arusha  limeteketea   kwa   moto  usiku  wa  kuamkia    tarehe 18 Novemba 2014  na kusababisha  hasara  ya  mabilioni  ya  fedha.

Wananchi  na  wafanyabiashara  ambao  vibanda  na  mali  zao   zote zimeteketea   wamesema walianza kupata   taarifa   za  moto  huo  usiku  wa kati ya saa  tatu  na saa   Nne    na   walivyofika   walikuta  kila  kitu  kimeteketea.

Wananchi  hao  wamesema  inakuwa  vigumu   kubaini  chanzo cha  moto huo  kwani   katika   eneo   hilo  ambalo  linamilikiwa  na  chama  cha  mapinduzi  (CCM) hakuna   umeme    wala   chanzo   chochote  cha  moto.

Aidha  wananchi    wameiomba serikali  na vyombo vinavyohusika   kufanya  uchunguzi   na   kuchukua   hatua   ya   kuwasaidia   kwani    ni   janga   kubwa     kwao  hasa   ikizingatiwa   kuwa   asilimia  kubwa  wanaendesha  biashara  zao   kwa   kutegemea mikopo.


Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET . 



Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X