Serikali imetangaza rasmi kuanza mpango wa kutengeneza barabara
zitakazotumiwa kwa kulipia kutoka Dar es salaam hadi Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo ya Serikali imekuja wakati foleni za barabarani zikizidi
kuongezeka kwa kasi katika jiji la Dar es salam jambo ambalo limekua
likilalamikiwa na wananchi.
Waziri wa Ujenzi John Magufuli alisema mradi huo utakua wa awamu
mbili ambapo ya kwanza itaanza Dar hadi Chalinze na nyingine Chalinze
hadi Morogoro.
Alisema sababu ya kuchukua uamuzi huo ambao umekua ukitumiwa na
nchi nyingine zilizoendelea duniani imechangiwa na tathmini iliyotolewa
ikionyesha kwa siku zinapita gari 56,000 katika barabara ya Morogoro.
“Kwa hali hii takwimu zinaonyesha kati ya mwaka 2015 hadi2016 magari
yatakuwa yakishikana kutokana na msongamano,ndipo tukafikiria utaratibu
huu ambao utasaidia watu mbalimbali wenye uwezo wa kulipia ili wasikae
katika foleni,”alisema Magufuli.
Alisema faida zitokanazo na utumiaji wa njia hizo utasaidia kuokoa
muda na kupunguza ajali barabarani na gharama kidogo za mafuta kutokana
na kuwa na mwendo kasi wa kilomita 120 kwa saa.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment