0
pinguWaandishi wa habari watatu walioshtakiwa kwa kuandika habari za kichochezi huenda wakaachiwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais.
Waandishi wa Habari hao Peter Greste raia wa Australia, Mohammed Fahmy mwenye asili ya Canada na Baher Mohammed wanashikiliwa Misri ambako walihukumiwa kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kukisaidia chama cha Muslim Brotherhood na kueneza habari za kupendelea upande wa Kikundi hicho.
Mohammed Fahmy, Peter Greste, Baher Mohamed
Rais wa Misri, Abdi Fatah El Sisi amesema msamaha huo utatolewa kama hakutakuwa na athari yoyote kwa nchi hiyo kiusalama.
Waandishi wawili kati yao walihukumiwa kifungo cha miaka 10, mmoja wao akihukumiwa kifungo cha miaka 7.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X