BAADA ya
msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka kuonekana akijiachia viwanja
mbalimbali tofauti na alivyokuwa akiishi awali, mzazi mwenzake, Malick
Bandawe, ameibuka na kumfungukia kuwa aachwe ajirushe.Malick alifungua
kinywa kufuatia madai kwamba alipokuwa akiishi na Rose alikuwa akimpa
sheria kali na kumkataza kwenda ‘out’ ndiyo maana alikuwa hajiachii kama
ilivyo sasa na hiyo ni moja ya sababu zilizosababisha uhusiano wao
kuvunjika.
“Mimi
siyo mkali wala sina sheria hizo ninazoambiwa ila nilikuwa nachukua muda
mwingi sana kuzungumza na Rose na ninaamini amejifunza mengi sana
mazuri ambayo akiyazingatia yatamsaidia maishani.
Msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Sababu
za Rose kujiachia hivyo ni kutokana na maisha ambayo tulikuwa tunaishi
hivyo anahitaji muda atatulia na atakuwa sawa na hapo ndipo atakapoanza
kuyafanyia kazi yale mazuri aliyoyapata kutoka kwangu, sitegemei yeye
kufanya mabaya ila nategemea afanye mazuri kwa ajili ya mtoto
wetu,”alisema Malick.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment