0

hadddd
UHURU
Mtoto wa kiume aliyezaliwa akiwa na mikono minne na miguu minne amesababisha sintofahamu mitaani nchini india kwa wenyeji kuamini kwamba ni mfano wa Mungu.
Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana’kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo ni jambo la kawaida kwa jamii za kihindu na watu wanasafiri kona mbalimbali za nchi hiyo  kwenda kumshuhudia mtoto huyo.
Polisi nchini humo wanalalamika kuwa wanafanya kazi kubwa ya kudhibiti makundi ya watu huku mamia kwa mamia wakilia mitaani kutaka kuingia ndani ya hospitali kumuona mtoto huyo.
Matatizo aliyonayo ya kuzaliwa na mikono miwili na miguu miwili ya ziada ni matokeo ya kutokua vema kwa mapacha walioungana.
Familia ya mtoto huyo imejawa na furaha kwa ongezeko la mwanafamilia mwingine na wanamuona mtoto huyo kama Mungu mtoto wa kiume wa familia ya Wahindu,Brahma ambaye anatambulika kwa kuwa na miguu na mikono minne.
UHURU
Wanafunzi wa chuo kikuu cha St Johns cha Mkoani Dodoma  wamegoma kuingia darasani na kuutaka uongozi wa chuo hicho kusikiliza kwanza matatizo yao yanayowakabili ikiwemo ukosefu wa vifaa katika Maabara.
Rais wa wanafunzi Damel Daniel alisema wamegoma kwa sababu za msingi zenye manufaa kwa elimu yao na kudai chuo hicho hakina vifaa vya Maabara kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na iliyopo haina vifaa kabisa.
Alisema uongozi umekua ukiwakomoa kwa kuwapunja alama katika mitihani yao na kuwarudisha nyumbani wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani huku kiwango cha ufaulu kikiwa wastani wa 50 kwenda juu.
Pia alisema kutokana na mazingira yasiyoridhisha baadhi ya walimu wamekua wakiacha kazi huku wengine wakiwa hawana uzoefu wa kufundisha katika vyuo vya elimu ya juu.
MWANANCHI
Polisi Mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmliki wa klabu ya usiku ya Linas Night Leornad Mtensa mwenye miaka50 ambaye anadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe alisema Mtensa ambaye alikua na mpenzi wake kwenye gari alifariki dunia kabla ya kufikishwa katika kituo cha afya cha ELCT Ndolage.
Alisema binti aliyekua naye kwenye gari anatokea Mkoani Mara na kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana baada ya gari lake kupekuliwa na kukutwa na vinywaji vya pombe kali vya aina mbalimbali.
Kamanda Mwaibambe alisema Polisi inamshikilia binti huyo ambaye inasemekana alikua mpenzi wa marehemu wakati upelelezi ukiendelea kwa kina kufahamu chanzo cha kifo chake.
MWANANCHI
Wakati kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali PAC ikianza kupitia ripoti ya IPTL kuhusu uchunguzi wa ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow ,wabunge wa kambi ya Upinzani wanaounda Ukawa umedai kwamba kuna mikakati  imeandaliwa kuzima ripoti hiyo isisomwe na kujadiliwa bungeni.
Mwenyekiti wa Ukawa James Mbatia alisema moja ya mikakati hiyo ni barua ya mahakama ya kuzuia mjadala huo akisema mkakati huo unatokana na ukubwa wa kashfa na jinsi unavyohusisha viongozi waandamizi wa Serikali.
“Iko mikakati na mbinu za kila aina kulihujumu bunge lisimamishe fedha za walipa kodi,ndio maana kuna danadana na tuna taarifa za kuwapo barua toka mahakamani kuzuia jambo hili lisijadiliwe bungeni kwa madai kuwa kuna kesi.”alisema Mbatia.
Pia alisema kuna taarifa kuwa Serikali inadai haina fedha  huku ikitaka kufupisha bunge na suala hilo lisijadiliwe kwa sasa..
MWANANCHI
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji ameingia katika mgogoro mpya baada ya kutuhumiwa kumpiga mbunge mwenzake  kutoka Tanzania Kessy Nderakindo jijini Nairobi,Kenya.
Bhanji ambaye amekua katika mgogoro na wabunge wenzake kwa kipindi cha miezi miwili sasa anadaiwa kumvamia Dk,Kessy na kumpiga mgongoni wakati kikao cha bunge hilo kilipoahirishwa.
“Kwa kuwa muda wa bunge ulikua umeisha nisingeweza kuipeleka kesi hiyo bungeni,badala yake kwa kuwa ni shambulizi nikaambiwa niende kuripoti kituo cha polisi cha Bunge ambapo baadaye nilipatiwa cheti cha matibabu”alisema Dk Kessy.
Hadi tukio hilo linatokea hakua amewahi kukwaruzana na Mbunge huyo zaidi ya kushangaa akimvamia na kusema baada ya kumvamia hakupata madhara ya hapo hapo kama alama ama damu ila anasikia maumivu katika sehemu alizompiga.
Bhanji hakupatikana kwenye simu yake na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu.
MWANANCHI
Taasisi ya Benjamini Willium Mkapa itafadhili vyuo vikuu kwa wanafunzi 890 kutoka Halmashauri 137 nchini ili kujiunga na vyuo vikuu93 vya afya katika mwaka wa masomo unaoanza 2014/16.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasis hiyo Ellen Mkondya  alisema ufadhili huo unalenga wanafunzi wanaosomea ngazi za vyeti  katika fani za Maabara,tabibu uuguzi na famasia na utagharimu  bilioni2.4.
Alisema miongoni mwa wanafunzi hao ,imejumuisha pia wanafunzi521 waliochaguliwa katika  vyuo vya Serikali na 327 wa vyuo binafsi na vya dini.
Alisema Taasis itatoa ufadhili kwa kulipia fedha  za uchangiaji kwa vyuo vya Serikali,wakati katika vyuo binafsi ufadhili utakua kwa asilimia50 ya gharama ya mafunzo.
JAMBOLEO
Jiji la Mwanza limegeuka uwanja wa vita baada ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo wanaodaiwa kuvamia eneo la msikiti wa Watanzania wenye asili ya Kiasia katika eneo la Makoroboi.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 5 asubuina kuendelea hadi saa10 jioni kwa askari polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kutanda katika maeneo ya msikiti huo.
Wafanyabiashara hao walidai kitendo kinachofanywa na Halmashauri ya jiji la Mwanza kuwanyima fursa ya kutafuta riziki zao kihalali na kudai eneo hilo si halali kufanya biashara huku wengine wakiruhusiwa kufanya biashara zao.
Walisema utaratibu wa kuwahamisha utafanyika ili eneo hilo libaki wazi nakusisitiza kama wao ni haramu hata eneo hilo la Makoroboi ni haramu maana wote wanavunja sheria na kanuni za jiji.
Walisema hawatakua tayari kupisha eneo hilo hadi wote waondolewe na haiwezekani wakafanye biashara eneo jingine ambapo wateja hawawezi kufika kununua bidhaa zao.
NIPASHE 
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limewatia mbaroni watoto wawili wajamii ya wafugaji wa kimasai kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na fimbo kichwani mkulima Nassor Mwinyiheri mwenye miaka45 mkazi wa Wilaya ya Handeni.
Watuhumiwa hao wenye umri wa miaka14 na mwingine 12 wakazi wa Wilaya ya Handeni wanadaiwa kumuua mkulima huyo kwa kumpiga na fimbo kichwani wakati akiwazuia kuingiza mifugo yao kwenye shamba lake lililopo kijiji cha Kwamagome.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Frasser Kashai alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa na wanakijiji wakisaidia na polisi baada ya kutokea mauaji hayo.
Vijana hao wanaatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni baada ya upelelezi kukamilika.
NIPASHE
Serikali imesema kuwa itatumia bilioni20 kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika December14 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri mkuu (Tamisemi) Kharist Luhanda alisema jana kuwa gharama hizo zitajumuisha tangu kuanza kwa zoezi zima la maandalizi ya uchaguzi huo mpaka siku ya upigaji kura utakapokamilika.
Alisema gharama nyingine ni kwa ajili ya kusafirisha masanduku,kulipa posho kwa watakaohusika na usimamizi wa uchaguzi,usafiri,kulipa wasimamizi wa uchaguzi na semina mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwa ajili ya elimu.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X