Ebola:Njia tano za kujiepusha virusi hatari vya homa ya Ebola
Ebola ni
mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia
hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
1. Sabuni na maji
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa
jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako
aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu
iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.
Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida.
Kusalimiana
kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan
International aliarifu BBC, kwani Ebola husambazwa haraka watu
wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua.
Dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika.
2. Hakuna kugusana
Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse.
Inaokena
kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka
kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na
kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji
ya uke- vyote huweza kueneza Ebola.
Dalili za
mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda
kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika,
na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia.
Tia watu hao moyo kutembelea kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Pia ni
uamuzi mzuri usiguse nguo au malaza ya waliougua Ebola- na Medecins Sans
Frontieres anashauri kuwa malazi ya waliougua yanafaa kuteketezwa.
3. Epuka miili ya wafu
Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko.
Baada ya
mtu kufa, bado unaweza kuambukizwa Ebola kutoka kwa miili yao kwani bado
inatoa maji maji ya mwili ambayo huweza kuwa hatari zaidi hata kuliko
ya mtu alieugua.
Fanya
mipango kupata timu ya magwiji kushughulikia mwili huo haraka
iwezekanavyo kwani ni hatari kuwacha mwili wa mfu kwa muda mrefu katika
eneo la makazi.
4. Usile nyama ya porini
Epuka
kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na
sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi
kwa binadamu.
Hata kama
mnyama fulani wa porini huliwa katika eneo lenu na nyama yake ni tamu
epuka myama huyo kwani nyama yake au damu yake huweza kuwa na virusi
hivyo.
Hakikisha vyakula vyote vinapikwa inavyostahili.
5. Usiwe na hofu
Kueneza uvumi huongeza hofu.
Usiogope
wafanyakazi wa huduma za afya- wako hapo kukusaidia na kliniki ndipo
mahali mwafaka kwa mtu kuponywa- wataongezewa maji na kutulizwa maumivu.
Takriban nusu ya watu walioambukizwa Ebola kufuatia mzuko wa hivi punde wa Ebola walifariki.
Kumekuwepo
na matukio ya madaktari kushambuliwa na watu kutorokwa wanaposhukiwa
kuwa na Ebola- hata wakati wanaugua ugonjwa tofauti.
Kuamini matibabu ya kiasili ambayo hayajathibitishwa kutoa afueni, pia kumechangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ebola.
"Kinga
ndiyo jinsi bora zaidi ya kukabiliana na Ebola, hivyo basi wacha uvumi
na usiwe na hofu; inawezekana kupunguza maumivu na kuokoa maisha,”
daktari Krishnan asema.
Ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD):
Dalili za Ebola ni homa, kufuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.
Maafa ya ugonjwa huu huweza kufika asilimia tisini- lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa 55% .
Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.
Hakuna
kinga wala tibaHuduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini
kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kuponaInafikiriwa kuwa
popo ndo vilemea vya ugonjwa huo.CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment