Hii ni moja ya mipango ya kampuni mpya ya simu iitwayo Viettel inayomilikiwa na jeshi la Vietnam inayojiandaa kuingia kwenye soko la simu Tanzania ambapo imemwambia Rais Kikwete juzi kwamba itateremsha kwa kiasi kikubwa bei ya simu za kawaida na smart phone ili kila Mtanzania awe na simu.
Imesema pia itasambaza mawasiliano ya Internet kwa kila kijiji Tanzania na taasisi za umma kama shule, hospitali na vituo vya Polisi, zitapatiwa huduma hii bila malipo yoyote.
Kingine walichokisema ni kwamba wanataka kupunguza bei ya simu za kawaida kufikia elfu 25 za Kitanzania na bei ya smart phone kufikia elfu 65 za Kitanzania ambapo pia wamekaririwa wakisema >>> ‘tunataka kuifanya bei ya kununua smart phone kuwa mara 10 chini ya bei ya kununulia computer, tunakusudia pia kupunguza bei ya matumizi ya simu kwa dola moja sawa na shilingi 1600 kwa watu wa kawaida kwa mwezi, kwa wale wanaotumia huduma nyingi zaidi watalipa shilingi elfu 78 kwa mwezi‘
Kwa kumalizia, unaambiwa ndani ya miaka mitatu ya kampuni hiyo kuanza kufanya kazi Tanzania, vijiji 4000 ambavyo sasa hivi havina mawasiliano vitapatiwa hiyo huduma kwa awamu ya kwanza.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment