Tumetoka
mbali! Picha ya staa wa Pozi kwa Pozi ‘PKP’, Omary Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’, aliyofotolewa enzi anaingia jijini Dar kwa treni imekuwa
kivutio kikubwa kwa mashabiki wake na sasa inaelekea kutapakaa kila kona
ya nchi na wengi wakibishana namna alivyokuwa awali na muonekano wake
wa sasa.
Huu ni muonekano wa Staa wa Pozi kwa Pozi, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kwa sasa.Picha hiyo ambayo ameipiga kitambo juzikati ilisambaa kwa kasi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuwafanya watu waanze kubishana kama ni yeye au ni mtu anayefanana naye na wengine kukerwa na picha hiyo wakisema itolewe kwa kuwa inamdhalilisha staa wao.
Baada ya kuona mzozo huo unakuwa mkubwa, blogg hiii ilimtafuta Ommy Dimpoz ili aeleze kama ni yeye ambapo alikiri kwamba ni yeye na kudai aliyekuwa na picha hiyo ni mjomba’ake tu anashangaa ilivyovuja mitandaoni.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment