
Dar es Salaam.
Mwanamuziki
 Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amesalimisha nguo zake za kijeshi 
kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Diamond
 alisema kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo 
(Oysterbay) akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa 
rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga 
kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu.
“Nisingeweza
 kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa 
kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa 
sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,” alisema 
nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika 
Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland.
Diamond 
alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli
 ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake 
kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa dhamana 
yoyote.CHANZO BONGO CLAN
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment