Hausigeli
aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya
kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu
kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji
machafu,
Mama wa Mtoto akiwa hospital baada ya kuzimia. |
Akizungumza
kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa
katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye,
alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu
aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo
alimkubalia na kumuagiza mboga.
Mama
wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na
mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa
kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea kwenye dimbwi la
maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
mwili huo
ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari
waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na
kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
Baadhi
ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa
marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo
alionekana kuwa na mambo
ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo
mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa
amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo
hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
Jumatatu
iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa
akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini
alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye
kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo
kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa
ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha
Chanzo Matukio na vijana
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment