Vanessa Mdee aka Vee Money amekanusha tetesi zilizopo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Nitasubiri’ Jux.
Siku za hivi karibuni, Vanessa na Jux wamekuwa karibu kiasi cha watu kuhisi kuwa ni wapenzi.
“Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda
sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu,”
amesema Vanessa aliyecheka baada ya kuulizwa swali hilo.
“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na
mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya
ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile
nyimbo ya Monefere.
"Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano Nahareel asingekuwa
na Aika basi nahisi na yeye pia wangesema hivyo. Ila sio hivyo
wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,” Amesema Vee .

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment