Kupitia Instagram ya Ray C ameandika:
Taasisi
ya Ray C Foundation iliyo chini ya muimbaji mkongwe, Ray C imefanikiwa
kuongeza mradi mpya wa mgahawa ambao utatoa fursa ya ajira kwa vijana
waliojikomboa kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Matunda ya Ray C Foundation,Namshukuru Mungu kwa kuendelea kutubariki,kupitia
foundation yetu tumeanza kufungua miradi mbalimbali ili kuwawezesha
vijana walioamua kubadilika na kuachana na dawa za kulevya kupata ajira
ili waweze kuendesha maisha!kwakuanza Ray C FOUNDATION imefungua mgahawa
nje ya hospitali ya Mwananyamala ili kuwawezesha wagonjwa na wauguzi
waweze kupata chakula cha kila aina na kitamu,mgahawa Wetu una chakula
cha kila aina na tunachukua oda za harusi,kitchen
party!msiba,birthday,mikutano nk.
Menu yetu
pilau Kuku,wali Kuku,wali nyama,pilau Kuku,pilau Samaki,ugali
Samaki,tambi na nyama ya kusaga,macaroni,beef
burger,Shawarma,sambusa,Bagia za kunde,chapati,ugali wa
muogo,kisamvu,bamia,mlenda,nyama chomaa,mbuzi choma,ndizi
choma,urojo,ndizi bukoba/mshale,vitumbua,juice ya miwa,juice ya
karoti,tikiti,juice ya avocado,.juice ya ukwaju,juice ya
mango!!!chocolate cake,cake ya zabibu kavu,chapati za maji etc agiza
chochote utaletewa hadi mlangoni pia tunafanya delivery
nyumbani,maofisini na mikutanoni .
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment