0

Said Fella akikabidhi msaada kwa wahusika wa hospitali hiyo.
Chege, Temba, Aslay pamoja na kundi zima la Mkubwa na Wanawe Jumatano hii walitembelea katika wodi ya watoto ya hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali. 
 Akizungumza na waandishi wa habari Said Fela alisema wanajisikia vizuri kutoa msaada kama huo kwakuwa na wao ni wagonjwa wa baadaye.“Tumeamua kuanza na watoto maana mimi ni mzazi na hata mke wangu anajifunguliaga hapa pia mimi nilikuwa mtoto na katika show yetu pengine wazazi waliopo hapa walipenda kufika lakini kutokana na kuuguza wakashindwa kufika. Na hii hatutofanya wilaya hii tu tukipata kingine kidogo basi tutapeleka na kwingine na hii isiwe sisi tumefunga milango wajitokeze na wengine kusaidia,” alisema.
Temba akiwa wodi ya watoto 
Aslay akiwa na wenzake 
Chege 

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X