MKONGWE wa muziki wa
kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, juzikati alinaswa akiwa na
demu mpya akiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika kwa 40 ya aliyekuwa
mzazi mwenzake, marehemu mama Tunda.

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’,akiwa na mpenzi mpya.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Septemba 21 mwaka huu ndani
ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati staa huyo aliyekuwa mmoja wa
watoa burudani katika tamasha la Fiesta, alipoonekana akiingia akiwa
ameambatana na mrembo mmoja akiwa ameshikana naye kimahaba.
Akiwa ndani ya uwanja huo, mkali huyo wa
mashairi yenye vina kwa muda mwingi alikuwa pamoja na msichana huyo
ambaye hakufahamika jina, wakiwa na dalili zote za wapendanao.

Mkali wa ‘Rhymes’ Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Afande Sele alicheka na kumtaka
paparazzi wetu kuachana na masuala hayo aliyoyaita binafsi, badala yake
asubiri apande jukwaani apate picha za kazi atakayofanya.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment