0


WATU nane, wengi wao wakiwa ni wa asili ya Asia, wanahofiwa kujeruhiwa vibaya kwa bomu lililotupwa kwenye mgahawa uliopo eneo la Gymkhana jijini Arusha usiku wa kuamkia leo. 
Jeshi la Wananchi likishirikiana na Jeshi la Polisi wanachunguza chanzo cha bomu hilo.

Hali ya wasiwasi imetanda mapema leo katika mji wa Arusha baada ya watu wanane kujeruhiwa, mmoja vibaya sana, kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mkahawa mmoja mjini humo. 

Afisa wa polisi Issaya Mngulu amethibitisha kuhusu kujeruhiwa kwa watu hao wanane lakini hakuna aliyekufa katika mlipuko huo. 

Mngulu pia amesema hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma hiyo

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X