Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kudai
kuwa ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na nyimbo za taarab, huku
akimtaka Khadija Kopa ajiandae.
Akizungumza na Sporah Show hivi karibuni, Ray C amesema kwenye albam
yake ambayo inakuja hivi karibuni kunamchanyiko wa nyimbo mbalimbali
zikiwemo taarab na zakihindi.“Nimefanya taarab kama mbili na zook, yani nimebadilishika kabisa, kuna kwaito , kuna bongoflave ,uwindi hindi kidogo, taarab nimeimba pia ,kwaiyo Khadija Kopa ajiandae”Alisema Ray C.

Pia Ray amedai kuwa aina ya muziki anaokujanao kwa sasa hivi ni ule wa kuonyesha kipaji chake zaidi cha kuimba na siyo kucheza.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment