RB nambari TBT/RB/3478/2014 ya Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar
es Salaam ina kesi ya dereva taksi aliyepatikana kwa jina moja la
Lindoya akidaiwa kuharibu mali za Asia Hakika kwa sababu eti alinyimwa
unyumba.
Akizungumza na Uwazi, Asia alisema: “Lindoya ni mpenzi wangu, tulikuwa tunaelekea kuwa mume na mke, maana tumeishi kwa miaka miwili sasa, lakini siku zote amenieleza kuwa hana mke wala watoto, lakini nimegundua kuwa alinidanganya.
“Ana mke na watoto wawili, nikaamua nimuache aendelee na familia yake. Akakataa, anataka kunitumia tu. Nilipomkatalia ndiyo akaamua kuniharibia vitu vyangu. Alinikuta nina vitu vya ndani nilivyonunua kwa fedha zangu, nimepanga chumba kwa pesa yangu na aliniomba tuishi pamoja nikamkubalia.
“Baadaye akaanza kujenga nyumba huko Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana niliamini kuwa tukioana tutakua tunaishi huko lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kujenga alimfuata mkewe huko Mbeya, wakahamia na watoto wake.”
Alisema, mpenzi wake huyo zilipendwa, alimwambia asikanyage nyumbani kwake kwa kuwa mkewe amekuja, jambo ambalo alikubaliana nalo kwa sharti kuwa wasitishe uhusiano wao lakini Lindoya akaonekana kutoridhika.
“Siku moja nikiwa kazini, alifika nyumbani kwangu akafungua
mlango kwa funguo wake, maana kila mmoja alikuwa na wake; akaharibu mali
zote ndani, akaacha kitanda tu. Nimeumia sana kwa kweli,” alisema Asia.
Kwa sasa kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Tabata kwa uchunguzi ambapo jalada la uchunguzi limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.



Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment