Mwili wa mwongozaji na mtayarishaji wa filamu nchini, George Tyson utaagwa katika Viwanja vya Leaders na baadaye utasafirishwa kwenda nchini Kenya kwa mazishi.
Akizungumzia
taratibu za mazishi, Awino Felix ambaye ni mdogo wake marehemu
Tyson alisema wanatarajia kuusafirisha mwili huo Jumatano ya
June 3 kwenda Nairobi Kenya baada ya kuagwa katika Viwanja
vya Leaders Club na kwamba marehemu atazikwa Kisumu, Kenya
Juni 7 mwaka huu.
Suzan Lewis "Natasha"
Suzan Lewis "Natasha"
Naye mama mkwe wa marehemu Tyson, Suzan Lewis "Natasha" ambaye ni mama mzazi wa msanii Monalisa amesema kuwa Tyson amefariki dunia akiwa na ndoto nyingi kichwani na kwamba hatamsahau kamwe katika kipindi chote cha uhai wake.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment