Home
»
KIMATAIFA
» MWEZI MMOJA TANGU NDEGE YA MALAYSIA KUPOTEA DALILI MPYA ZAONEKANA
Kisanduku
cheusi cha sauti cha ndege ya MH370 ya Malaysia Airlines iliyopotea kwa
zaidi ya majuma matatu, kimeshukiwa kuwa chini ya maji, kwa sasa zoezi
la kuitafuta ndege hio limehamia chini ya maji baada ya meli moja ya
Uchina inayoshiriki kwenye zoezi hilo kubaini ishara ya sauti ambayo
huenda ikawa imetoka kwenye kisanduku cheusi cha ndege hiyo.
Kufuatia
taarifa hizo, tayari uchunguzi umeanza kuhusu eneo ambako sauti hizo
zilibainika ingawa ni sehemu tofauti kabisa na ile ya awali ambayo
ilionekana kwenye picha za Sattelite za nchi ya Australia na China.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment