
Kwa mujibu wa chanzo chetu Papaa huyu alikuwa akisakwa muda mrefu sana, ata wakati anafunga ndoa na Aunt Ezekiel alikuwa akiishi kimashaka mashaka kwa kuogopa kuingia katika mikono ya dola ya waarabu hao. Papaa huyu mwenye kupenda kuwa na mabinti wa kitanzania ambao ni maarufu, chanzo kilienda mbali zaidi na kututanabaisha ya kuwa pia amewahi kuwa na mahusiano na baadhi ya wasanii wa kike waliowahi kukata nyonga katika moja ya bendi maarufu hapa jijini Dar es salaam. Mtandao huu umejitahidi kumtafuta Aunt Ezekiel ili kumuuliza kama taarifa hizi anazo, ila simu yake haikupatikana mpaka tunaingia mitamboni, vile vile mtandao wako unajaribu kuwasiliana na mwakilishi wetu wa serikali nchini humo Bwana Omary Mjenga ili kuweza kujua kama wana taarifa yoyote ya kukamatwa kwa mtanzania huyu na nini wanatakiwa kufanya ili kuweza kujua chanzo kikuu na nini hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa za kuweza kumsaidia.
Taarifa zaidi tutawajulisha pindi tutakapowapata watu wengine ambao tunawatafuta ili kuweza kujua ni nini cha kufanya ili kumuwezesha atoke na kuweza kuishi salama salmin.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment