WATU 13 aiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku wa kuamkia leo.
Ajali hiyo
ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga
mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi
wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima
ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao
pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo
hilo.
Basi hilo
lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo
mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi,
Singida.
Miili 14 ya
waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya
Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini
hapo.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment