Jamaa aliyejitambulisha kwa
jina la Salum Athuman (22), amejikuta akivishwa kanga na kutembezwa
mitaani baada ya kwenda nyumbani kwa mwanaume mwenzake, Dastun Mkereti
(26) kwa lengo la kujivinjari na mke wa mtu, Stela Ramadhan (20),
akafumaniwa.
Tukio hilo lililofunga mitaa lilijiri maeneo ya Temeke, Dar, hivi karibuni na kugeuka sinema ya bure.
Ilidaiwa
kuwa jamaa huyo amekuwa akimsumbua mkewe kwenye simu kwa kutaka waonane
ili wavunje amri ya sita huku akijua fika kuwa Stela ni mke wa mtu na
alishapewa onyo mara nyingi na mwenye mke.
Ilielezwa
pia kuwa cha kushangaza, pamoja na mwanamke huyo kubadili namba ya
simu, wiki iliyopita jamaa alimpigia Stela kisha akamsisitiza waonane,
ikibidi alale naye siku nzima kwa kuwa alikuwa anataka kukumbushia enzi
zao kwa sababu aliwahi kutoka naye kimapenzi, kipindi cha nyuma kabla
hajaingia kwenye ndoa.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment