Hatimaye
baada ya mvutano wa baadhi wa wajumbe wa Bunge
la Maalum la Katiba kuhusu upigaji wa
kura ya siri na ya wazi kuendelea leo Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni
na Haki za
Bunge Maalum, Mhe . Pandu Ameir Kificho amewasilisha azimio la
mapendekezo ya ya upigaji kura wa wazi na siri kutumika kwa pamoja
katika kaununi ya 37 na
38, ambalo limetipitishwa na Bunge hilo kwa matokeo ya
jumla kwa kura ya ndiyo 376 na
hapana 133 .
Kura
hizo zimetangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge ,hilo, Mhe.Samia
Sululu kabla ya kuahirisha kikao hicho leo usiku, ambapo alisema
azimio
hilo limepitishwa na Bunge hilo , kufuatia
upigaji wa kura ,ambapo idadi ya kura
zilizopigwa ni 509, wakati
mauhudhurio ya wajumbe yalikuwa 511.
Mhe
. Samia alisema kwa upande wa kura za wazi zilizopigwa ni 438,
ambazo za ndiyo zilikuwa 351 na hapana ni 87, wakati kura za siri
zilizopigwa zilikuwa ni 71, ambazo za ndiyo zilikuwa 25 na hapana ni
46.
Uamuzi
huo umefuatiwa
baada ya hali hiyo ambayo
ilitokea tena kwa mara nyingine jana jioni mara baada ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Kanuni
na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Kificho kuwasilisha mapendekezo ya
upigaji kura wa wazi na siri kutumika kwa pamoja katika kaununi hizo.
Tangu jana jioni na leo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakitoa michango kutaka
upigaji kura huo uwe wa wazi na siri , huku wengine kutaka kura ya siri.
Awali Kanuni za 37
na 38 zilibaki kiporo tangu wakati wa
utungaji wa kanuni mbalimbali za Bunge
hilo, na uchangiaji wa kuziboresha, kutokana na mvutano huo,
ambao baadhi ya wajumbe kutaka kura ya
uwazi na wengine siri.
Wakizungumzia juu ya makubaliano yaliyofanywa na Kamati ndogo
ya Muda ya Maridhiano na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge kuhusu mapendekezo ya upigaji kura huo.
Mmoja ya wajumbe wa Kamati hiyo ndogo ya Maridhiano, John
Nyika alisema walifanya mazungumzo hayo
waliona ni vema wakubaliana mtu anayeweza kupiga kura ya uwazi na anayetaka ya siri wapige kulingana na
matakwa yao ili kuwezesha mchakato huo
kupiga hatua mbele.
“ Tunaomba utaratibu huu wa maridhiano uendelee
… ili tuweze kupiga hatua mbele,” huku akisisitiza hawana dhamira
yoyote ya kukwamisha mchakato wa Katiba
mpya. Hivyo watakuwa wa kwanza kuunga mkono kwa kura azimio litakalopitishwa
kwa kura zitakazokubaliwa.
Naye mjumbe mwingine wa kamati hiyo , Vuai Ali Vuai alisema
jambo hilo ni kubwa kwa Watanzania ndio
maana wanatakiwa kupiga kura kwa uwazi umma uweze kuona .
Kwa upande wake ,mjumbe
mwingine wa kamati hiyo ya ndogo ya Maridhiano
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela
amesema ni vizuri wajumbe hao
wakakubali azimio hilo kwa kuwa mpaka sasa wameshatumia siku 40 kujadili kanuni
za kuongoza Bunge hilo na zimetumia gharama hivyo wasiendelee kuongeza gharama,
zipo siku tatu za kuomba ili kufanikisha maridhiano hayo.
“ Ninawaomba wajumbe wenzangu kukubali azimio hili ili
tuweze kusonga mbele na na mchakato wa kupata Katiba ,” alisema Askofu
Mtetemela.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment